ANTONIO CONTE: TETESI ZA KUFUKUZWA KAZI NA CHELSEA ZINANICHEKESHA SANA
Kocha wa timu ya Chelsea yenye maskani yake Stamford bridge nchini Uingereza , Antonio Conte asema taarifa za kusimamishwa kazi na uongozi wa chelsea zinamfurahishaga sana.
Kocha wa Chelsea Antonio Conte
Wacheza kamari wengi wametabiri kwamba Antonio Conte atasimamishwa kazi na Chelsea kufuatia matokeo mabaya katika mechi zake nne za mwisho. Chelsea ilianza vizuri ikishinda michezo yake mitatu ya mwanzo ya ligi kuu Uingereza, lakini mambo yamekuwa ndivyo sivyo katika michezo iliyofuatia kupelekea kushuka katika msimamo wa ligi kuu mpaka nafasi ya saba.
Mitandao mingi ya michezo leo imetawaliwa na mjadala wa nafasi ya Antonio Conte kwenye timu ya Chelsea ikiwa ina kibarua kizito cha kuwakabili mabingwa wa msimu uliopita Leicester city.
"Ni ngumu kuongelea nafasi yangu kwasababu nimejikita katika kuitengeneza timu na kupata matokeo mazuri, nina mawasiliano mazuri na klabu na ninajitahidi kutatua makosa ya msimu uliopita kwa ajili ya siku za usoni" alisema kocha huyo.
Kwenye mchezo wa leo kiungo mkabaji Ng'olo Kante ataikabili timu yake ya awali Leicester city kwa mara ya kwanza tangu alipoihama klabu hiyo kwa dau la uhamisho la £30m.


Eheeee apo sasa
ReplyDelete