MAMBO 10 AMBAYO MWANAUME UPENDA KUSKIA KWA MKEWE LAKINI ASIYATAJE




 Mambo 10 Ambayo Mwanaume Hupenda Kusikia Toka Kwa Mkewe au Mpenzi Wake kwa sababu Mapenzi ni kitu kizuri na ni jambo la furaha watu wakipendana lakini pia swala la kuwa mbunifu katika kumjali mumeo ni swala ambalo ni muhimu sana kwa kufahamu nini anapenda na kitu gani hapendi ni jambo ambalo unaweza kudumisha ndoa yako na kuifanya kuwa ya mda mrefu na yenye furaha na ndio maana kuna mambo mwanaume anaweza akaitaji kuyaona kwa mke wake lakini asiulizie kwa kumpima mkewe kama ana jali au hajali. Na ndio maana anko wenu leo nimewaletea jambo hili ambalo lipo katika jamii na mngependa kufahamu sasa kaa na mimi tuyachambue mambo haya


10. Kuwa muwazi kwenye kusema makosa.

Wanaume wanaweza kujikweza sana lakini daima hawachukii kurekebishwa na pia wanaume wengi pale anapokosea mwambie kwa lugha ya pole pole yenye chembe za uba ndani yake na ni sumu kukaa na kitu moyoni alafu yashajirundika siku mmegombana ndio unaanza kuyavurumisha moja baada ya lingine hii kitu uchukiza wanaume wengi, kosa limetokea sema na sio kununa bila sababu kwa kuficha vitu moyoni uyo ni mtu wako wa milele usipomwambia ukayapeleka kwa marafiki unajimaliza mwenyewe.
9. Kupeti petiwa

Wanawake wengi hutaka wao tu ndio waulizwe kuhusu jinsi siku zao zilivyoenda kila siku, wanasahau kabisa hata wanaume nao walikua kwenye mihangaiko. Mzoeshe kumuuliza mpenzi wako siku yake ilikuwaje? utaona hata nuru ya mapenzi yenu itang’aa na mtakua marafiki, japo mwanzoni atakua hakuambii kila kitu lakini baada ya muda atazoea. Kila mtu anataka wa kumsikiliza, mtu atakayezungumza nae chochote kilichotokea ndani ya siku yake, na pengine kukuuliza ushauri.
8. Kusali na kumcha Mungu
Ujue sifa moja ambayo Mwanaume anaweza kuwa nayo anaweza kuwa mtu asiesali lakini upenda kumuona mkewe anasali na kitu kinacholeta ugomvi siku hizi ni wanandoa kutaka kwenda sawa kwenye kila jambo na wengine kusahau nafasi zao na mwanamke anaesahahu nafasi yake mwanaume umuita kiburi kwa kupenda kuwa sawa kwenye kila jambo na wanaume wengi uamini kwenye matendo sana kuliko kusali nadhani ni kutokana na mambo mengi waliowai kukutana nayo na kuyaona ila jambo la kumcha Mungu ni jema ambalo mume akiliona kwa mkewe ufarijika sana. Mwanamke mcha Mungu siku zote huwa ni wazo la kila mwanaume endapo ana mpango wa kuoa. Mwanaume huwa na amani kwa kiasi fulani akiongozwa na mwanamke wake kwa upande huo wa sala.
7. Kuomba  Msamaha

Katika kila ndoa au mahusiano ya kawaida unapokosea na kuomba msamaha Mwanaume yoyote upenda kuskia ivyo na itakuwa vizuri zaidi kama utatamka na lile kosa lako ulilotenda na kuomba msamaha kwa kumtaja kwa cheo cha mume wangu nisamehe nimekukosea sana na sikupaswa kufanya ivyo, Vinagongana vikombe sembuse nyinyi wanandoa hamna mtu ambae amekamilika katika dunia hii kila mtu ana mapungufu yake cha msingi ni kufahamu mampungufu ya mwenzio na kufanyia kazi na mengine kuvumiliana.Usililete tena mezani jambo ulilosema umesamehe.
6. Kushukuru na kutoa ya Moyoni Kama amefanya kazi nzuri, mwambie. Wote tunajua sio kila siku sio jumapili na sio kila siku watu uonyesha uwezo wa messi na siku mtu akiwa kwenye kiwango kizuri hufahamu kwa hyo kumshukuru kwa kueleza ya moyoni ni jambo jema sana na jitaidi usiwe mkali katika hili mwambie kwa sauti ya mahaba ya taratibu ata alipokosea pia sema kwa utaratibu kwa sababu wanaume wengi uamini wanawake ni watu wapole wenye semi za taratibu na ni mwiko kumfanya aamini vinginevyo.
5. kuitwa majina mazuri na upekee

Kuna baadhi ya maneno mwanaume anaweza asikwambie lakini utamani kuyaskia kutoka kwako mfano: Katika maisha yangu kuna wanaume nimekutana nao sikatai baby lakini wewe umuimu wako katika maisha yangu nashindwa ata kueleza kwa jinsi ulivyo nikaa moyoni mume wangu naomba usinipe tabu ya kuanza maisha mapya na mtu mwingine mume wangu" katika kutamka maneno haya usisahau viunganishi vyenye mashiko kama neno mume wangu, mwandani wangu au mpenzi wangu uleta tija sana kuliko maneno ya kingereza uonekana ni ya kawaida Jua kumsifia mwanume na atakuweka kwenye nafasi muhimu sana.
4. Kuaminiwa

Mwanaume upenda kuaminiwa japo inapotokea anaaminiwa sana ujisahahu pia nafikiri mwanaume ukimwamini usimwambie acha matendo yajioneshe na hata kama anafanya uchafu wake atajiskia aibu na ufurai kuona kama mwanamke unacheza kwenye nafasi yako vizuri bila kumpanda kichwani au kupenda kumkaripia wanaume wengi hawapendi kukaripiwa na hasa wakiwa na marafiki zao huisi wamevunjiwa sana heshima mwengine anaweza asikwambie ila akakushusha vyeo katika mahusiano yenu. Japo wengine hulitumia hili kwa uchafu wao lakini wengi wao ni kitu chema kwao.
3. Kujiongeza katika tendo.
Ni mtazamo wa wengi kwamba mwanaume ndio siku zote awe mwanzilishi wa tendo. Lakini mwanaume kwa wakati mwingine hupenda mwanamke wake ampe vishawishi na yeye vya kumleta kwenye mood. Sio kila siku aanze yeye tu, wakati tendo ni la kuwafurahisha wote. Hata kama ni ngumu kusema kwa mwanamke, ishara kibao zipo za kumuonyesha mwenzi wako akaona ‘Leo baby anataka na yeye’.
2. kuuliza mambo yenye tija katika ndoa.

Lengo la kila mwanaume ni kupata mwanamke alie sahihi katika maisha yake ambae anajua nini maana ya maisha ndio maana wanaume wengi hupenda kuringishia wake zao kwa marafiki na kigezo kikubwa huwa ni akili alionayo mwanamke mfano " mama Ally anajielewa sana yule mwanamke kila siku lazma aniingizie kitu kichwani mwangu nafurai kuwa nae" Na pia upenda kuulizwa nini ndoto au malengo yake katika maisha na sio mwanamke ambae mnakaa tu bila kuulizwa maswala ya msingi au kumpa changamoto yoyote ya msingi mwanaume kwa kufanya haya kama mwanamke utajiwekea nafasi nzuri kwenye moyo wa mumeo na atakuamini katika mambo yake makubwa
1. Maneno mazuri yenye kutia moyo
Wanaume wengi hujiona wagumu kwenye kutamka neno ‘I love you’ kwa wanawake zao na hata akisema itakua ni mara chache chache hata kama kweli kutoka moyoni wanapenda, lakini haina maana hawataki kuambiwa na watu wanaowapenda, hii huwaaminishia nafasi yao kwenye moyo wa mwanamke. Na wanavyosema wanaume wanapenda kudekezwa japo ni wakali ni kweli ata mbwa akiwa mkali vipi ukimuita jina na kumkuna manyoya mwenyewe analala chini na kufuraia jambo hilo cha msingi tusiwe wavivu kujaribu kumjali mtu inasaidia sana.

Usisahau ku comment na ku share kama umeipenda story hii mdau wangu au unaweza kunitumia ujumbe wako kwenye email: dingadrizzy@ymail.com

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.