LEICESTER CITY YAPAA, TIZAMA HAPA MATOKEO YOTE YA LIGI YA MABINGWA ULAYA JANA USIKU


Hapo jana katika mechi za michuano ya barani ulaya ngazi ya vilabu, Leicester City wamezidi kuwa mwiba mchungu baada ya kuwachoma mabao 2 - 1 Club Brugge kutoka ubelgiji. Mabao ya Leicester yaliwekwa kimyani na Shinji Okazaki baada ya kumalizia kazi kubwa iliyofanywa na Fuchs. Na bao la pili Mualgeria Riyad Mahrez aliifungia Leicester kupitia mkwaju wa penalty. Kocha wa timu hiyo Claudio Ranieri anaamini kikosi hicho kitafika mbali katika michuano hiyo ya Ulaya.
Nayo Borussia Dortmund hapo jana imekuwa timu ya nne kufunga magoli nane katika mchezo mmoja katika michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya baada ya kuilaza legia warsaw mabao 8 - 4.


Nimekuwekea hapa na matokeo ya mechi zote za ligi ya mabingwa jana usiku.

Monaco 2-1 Tottenham
Borussia Dortmund 8-4 Legia Warsaw
Sporting 1- 2 Real Madrid
CSKA Moscow 1- 1 Bayer 04 Leverkusen
FC Copenhagen 0-0 FC Porto
Dinamo Zagreb 0-1 Olympique Lyonnais
Sevilla 1- 2 Juventus

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.