YOUTUBE: TAKWIMU ZINAONESHA MUZIKI WA TANZANIA NDIO UNAOTAZAMWA ZAIDI NCHINI KENYA
Video za muziki wa Bongo Flava
kutoka Tanzania ndizo zilizotazamwa zaidi na Wakenya katika mtandao wa
YouTube, unaomilikiwa na Google, mwaka huu, takwimu zinaonyesha.
Video
hizo zinatawala katika orodha ya video kumi zilizotazamwa zaidi,
inayoongoza ikiwa video ya wimbo Salome, uliofanywa upya na Diamond
Platnumz na Rayvanny.
Wimbo wa Work, wao Rihanna na Drake ni wa
pili lakini kutoka hapo anaingia Diamond Platnumz na Harmonize wakiwa na
wimbo wao Bado.
Video ya kwanza ya Wakenya kwenye orodha hiyo ni ya Sauti Sol kwa wimbo
wao Unconditionally Bae, lakini bado kwenye wimbo huo walishirikiana na
mwanamuziki Mtanzania, Alikiba
Hii ni hatua nzuri kwenye muziki wa bongo kwani inatoa matumaini na mwangaza kwamba ndio muziki unaokubalika zaidi Afrika Mashariki.


Leave a Comment