JINSI KUFANYA MAOMBI YA UHAMISHO KUTOKA CHUO AMA KOZI NYINGINE NACTE BAADA YA KUCHAGULIWA
Maombi ya Uhamisho
Mwombaji aliyechaguliwa ataweza kuomba uhamisho kutoka chuo ama kozi moja kwenda nyingine kupitia kwenye ukurasa wake binafsi (profile) tu. Uhamisho huu utategemea nafasi zilizopo, ushindani na alama za chini za kujiunga na kozi (cut-off).
Hatua za kuomba uhamisho:
Mwombaji aliyechaguliwa ataweza kuomba uhamisho kutoka chuo ama kozi moja kwenda nyingine kupitia kwenye ukurasa wake binafsi (profile) tu. Uhamisho huu utategemea nafasi zilizopo, ushindani na alama za chini za kujiunga na kozi (cut-off).
Hatua za kuomba uhamisho:
- Ingia kwenye ukurasa wako binafsi (profile) kwa kutumia jina la mtumiaji (Username) na neno la siri (Password) ulivyopewa wakati wa usajili.
- Bofya kitufye kilichoandikwa “Transfer Request/Kuomba uhamisho”, na punde ukurasa utafunguka
- Utafunguka ukurasa unaokuonesha chuo na kozi uliyochaguliwa awali
- Chagua kada unayohitaji kuhamia
- Chagua chuo unachohitaji kuhamia
- Chagua kozi unayohitaji kuhamia
- Mfumo utatathmini kama una sifa za kujiunga na kozi uliyochagua. Iwapo una sifa za kujiunga na kozi hiyo mfumo utakuomba ulipie Sh. 30,000/- kama ada ya maombi ya uhamisho. Kiasi hiki hakitarudishwa (non-refundable)
- Bofya kitufye kilichoandikwa “Confirm Transfer Request/Kamilisha maombi”.
- Utapewa muhtasari wa maombi yako ya uhamisho pamoja na kutumiwa ujumbe mfupi wa maandishi kwenye namba ya simu ya mkononi uliyoweka wakati wa usajili na barua pepe kukujulisha kwamba umekamilisha maombi.
- Piga *150*00#
- Chagua 4. LIPA kwa M-Pesa
- Chagua 4. Weka namba ya kampuni
- Tafadhali weka namba ya kampuni (No. 607070)
- Weka namba ya kumbukumbu ya malipo (No. 1234)
- Weka kiasi (e.g.30,000/=)
- Weka namba ya siri
- Bonyeza 1 kuthibitisha.
- Kuhama chuo na kozi si lazima.
- Uhamisho utafanyika kwa kozi zile tu zenye nafasi na kwa vyuo ambavyo bado havijafunguliwa na kuanza masomo.
- Uhamisho ni kwa wale waombaji waliokwisha kuchaguliwa kupitia mfumo wa pamoja wa udahili tu.
- Maombi ya uhamisho yanaweza kufanyika MARA MOJA na kwa kozi moja
- Iwapo umefanikiwa kupata uhamisho, majibu yataonekana kwenye ukurasa wako binafsi (Profile). Majibu haya pia yatatumwa kwenye namba yako ya simu kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi na kupitia barua pepe baada ya tarehe ya mwisho ya maombi (15 Oktoba 2016).
- Uhamisho utategemea ufaulu wa waombaji na nafasi zilizopo. Hii inamaanisha kwamba wenye ufaulu wa juu ndio wenye uwezo mkubwa wa kukubaliwa kuhama.
- Maombi yatakayo tumwa kwa barua au barua pepe hayatoshughulikiwa.
SOURCE: Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)
Leave a Comment