ULIMAJI WA MATIKITI MAJI NA SHUHUDA HALISI ZA FAIDA ZAKE
Mahitaji
1. Shamba la eka 5
2. Mbegu
3. Gharama za uendeshaji wa shamba
Matikiti maji aina ya Sugar baby yanachukua siku 60 toka
kupandwa hadi kuvuna na kwa mwaka unaweza kulima mara 4 .
Upandaji:
Nafasi ya shimbo moja kwenda lingine ni 2mx2m na kila shimo unatakiwa
kuweka mbegu 2 ambazo zinazaa matunda 2 - 3 ambayo wakati wa mavuno
hukupatia matunda 4 -
6
Hivyo kwa spacing hiyo napata
mashimo 1000-1200
Idadi ya matunda
Mashimo x Matunda kwa shimo x ekari 1,000 x 5 x 5 = 25,000
Mapato
Wastani wa shilingi 500 kwa tikiti x idadi ya matikiti kwa
eneo la ekari 5 25,000 x 500 = 12,500,000
Mapato kwa mwaka
12,500,000 x 4 = 50,000,000
Gharama za uendeshaji wa shamba kwa mwaka ni Tsh 25,000,000
MKULIMA WA MATIKITI NA USHUHUDA WAKE
kwanza hongera kwa kuamua kuingia shambani, mimi nalima matikiti na nimeshajitoa kulima ktk kipindi hiki cha masika, kubwa zaidi tafuta mbegu bora kwenye maduka ya kilimo mfano pitia kariakoo, mimi nalima Hybrid F1 sugar queen, na kiwango cha ekari moja utatakiwa kuwa na gram 300 na kila shimo panda mbegu 2 japo wapo wanaopanda mpaka 3, na hapa utatakiwa kuwa na mshimo kama 2000.
Andaa shamba vizuri japo wiki tatu kabla ya kupanda na hakikisha eneo lako lina maji ya kutosha kwani tikiti linahitaji maji mengi katika uhai wake, Panda kwa mbolea, ni vema zaidi kama utapata samadi na kama utatumia ya viwandani zipo kama vile winner(hapa kuna kiambato chake, utamuuliza muuzaji), kwa kukuzia utatumia CAN, andaa dawa za wadudu wanaokata majani pindi matikiti yanapoanza kuota tu na pindi unapoona dalili za matikiti kushambuliwa majani (karate itakufaa).
Unahitaji uangalizi wa karibu sana kuanzia mwanzo mpaka mwisho na hakikisha unakuwa na dawa za kutosha kwa ajili ya kuzuia wadudu waharibifu, ukungu hasa kipindi hiki na magonjwa yanayoshambulia majani, maua na matunda.
Gharama kubwa utakayoingia kwenye kilimo hiki ni kwenye mbegu( ekari moja ni gram 300= 250,000 kwa Dar), dawa( hapa inategemea na hali ya eneo na jinsi magonjwa na wadudu wanavyoshambulia), nguvu zako mwenyewe kwenye kumwagilia( hapa kama unatumia ndoo, ila kama unatumia mashine ya kuvutia maji basi utahitaji wastani wa lita 5 kwa ekari moja kila unapomwagilia) na kutunza shamba, kama unatumia kijana basi hapo ni makubaliano yenu, bomba la kupigia dawa ni muhimu sana.
Mavuno ni kuanzia siku 65 mpaka 75 inategemea na eneo lenyewe na aina ya mbegu, na kiasi cha mavuno kwa ekari moja ni kiasi cha matikiti kama 7000( kila mche mmoja utoe matikiti 2 tu yenye afya nzuri) na soko likiwa nuri basi utauza kwa wastani wa Tsh 1500 au zaidi shambani, na ukiMU kwenda mwenyewe sokoni mfano Buguruni unaweza kuuza bei nzuri kama ni kipindi mmea huo haupatikani.
Ushauri: usiende shambani na matarajio makubwa zaidi ya kupata hela nyingi ukasahau changamoto zake( mavuno kidogo, hasara na muda), shambani kunahitaji uangalizi wa karibu sana na usijaribu kulima kwa simu hasa kama una watu wasio waaminifu watakuua kwa ugonjwa wa moyo. Pia hizo faida zinazopatiakana ni pale tu utakapo fata ushauri wa kitaalamu na ukaamua kwa dhati kufanya kilimo.
Karibu tulime.
Nashukuru nimeipenda hii
ReplyDelete