IJUE SHERIA: MTU AU CHOMBO CHENYE MAMLAKA YA KUMKAMATA MTUHUMIWA




 
Taratibu za nchi kupitia sheria mbalimbali zimeweka bayana mtu au chombo chenye mamlaka ya kumtia mtu nguvuni. Kwa mujibu wa taratibu za nchi ya Tanzania, wafuatao ndio wenye mamlaka ya
kumtia mtu nguvuni:
a. Askari polisi,
b. Mgambo na Sungusungu
c. Mtu binafsi,
d. Hakimu wa Mahakama yeyote.


Kwa kawaida, mtuhumiwa anakuwa ametiwa nguvuni pale atakapozuiliwa na polisi na kuondolewa haki yake ya kwenda atakako. Lengo kuu la kufanya hivyo ni kumweleza mtuhumiwa kosa analotuhumiwa nalo na pia kutoa mwanya kwa mamlaka yaani polisi au chombo kingine kama vile TAKUKURU kufanya upelelezi wa kutendeka kwa kosa la jinai. Mtuhumiwa anapokuwa ameshukiwa kuhusika katika kutenda kosa, na wakati askari polisi anapokuwa akifanya kazi ya upelelezi wa kosa la jinai anayo mamlaka ya kumzuia mtuhumiwa kwenda atakako hata kama polisi anayehusika na zoezi hilo hana uhakika kama mtu anayemzuilia ametenda kosa husika au anahusika katika kosa hilo. Mtu atahesabika kuwa ametiwa nguvuni ikiwa atazuiliwa kuondoka na kwenda atakako kutokana na kuwa nguvuni; au kutendeka kwa kosa la jinai na polisi anaamini kwamba mtu huyo ametenda kosa hilo la jinai. Katika mazingira haya, sheria inampa polisi mamlaka ya kumkamata mtu huyo bila ya kuwa na hati ya kumkamata. Mazingira yafuatayo yanampatia mtu binafsi au askari polisi haki ya kumkamata mtuhumiwa bila ya kuwa na hati ya kukamata (Warrant of Arrest)


a. mtu atakayefanya tendo la kuvunja amani mbele ya askari,


b. mtu anayemzuia askari polisi kufanya kazi zake, au atafanya jaribio la kutoroka au atatoroka kutoka chini ya ulinzi,

c. mtu atakayeonekana kuwa na mali ya wizi au inayoshukiwa
kuwa ya wizi,


d. mzururaji au mtu anayezurura kwa nia ya kufanya uhalifu,


e. mtu anayeshukiwa kuwa hati ya kukamatwa imeshatolewa
dhidi yake,


f. mtu yeyote ambaye amefanya kosa nje ya Tanzania na kuna uwezekano wa kuadhibiwa ndani ya Tanzania,


g. mtu anayedharau nembo ya taifa kama vile wimbo wa Taifa au Bendera ya Taifa Endapo mtuhumiwa atakamatwa na raia, basi ni wajibu wa raia kumfi kisha mtuhumiwa mbele ya kituo cha polisi haraka iwezekanavyo.

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.