SHERIA: JINSI YA KUJIKWAMUA MAHAKAMANI NA HAKI ZAKO KAMA RAIA KWENYE KOSA LA JINAI



Posted by Erasto Odiero
17 October, 2016

Makosa  ya  jinai  ni  makosa  yote  yaliyoorodheshwa  katika  sura  ya  16  ya  kanuni  za  adhabu  pamoja  na  yale  yaliyo  katika  sheria  nyingine  kama  ile  ya  uhujumu  uchumi.  Pamoja  na  kuwapo  sheria nyingine  ambazo huorodhesha  makosa  ya  jinai   bado  Kanuni  za  adhabu  inabaki  kuwa  sheria  kuu  inayoorodhesha  makosa  ya  jinai.  Kwa  ujumla  katika  sheria tunayo makosa  makuu  ya  aina mbili. 

Kwanza  ni  hayo  ya  jinai  na  pili  ni  ya  madai.  Kwa  kusema  makosa  ya  jinai  na  madai  unajikuta  umeongelea  karibia  makosa  yote unayoyajua  na  usiyoyajua.  Kila  kosa  unalolijua  kichwani  mwako  lipo  katika   moja  ya makundi  haya.

Kwa  mifano  tu  makosa  ya  jinai  ni  kama  kupiga,  kutukana, kuendesha  kwa  uzembe( ulevi, kuongea  na simu, mwendo  kasi,kuzidisha  abiria n.k), kudhalilisha, kuiba, kubaka, kuua, utapeli, kughushi, ufisadi, rushwa, matumizi  mabaya  ya  ofisi  ya  umma, kulawiti, kumiliki  madanguro, ukahaba, dawa  za kulevya( kutumia au kuzimiliki), kuzuia  mahakama  au  mamlaka  za  kisheria  kutekeleza  wajibu, kuharibu  mali  ya  mtu, kuvamia eneo  la  mtu  kwa  nia ovu, manyanyaso  ya  jinsia  na  mengine  mengi.

.
Haki za raia au Mtuhumiwa wa Kosa la Jinai

i. Kila mtuhumiwa wa kosa lolote la jinai anahesabiwa kuwa hana hatia hadi hapo chombo chenye mamlaka (mahakama) ya kuzisikiliza tuhuma kitakapomsikiliza na kumuona na hatia dhidi ya kosa analotuhumiwa.


ii. kila mtuhumiwa ana haki ya kuthaminiwa utu na heshima
yake au kutoteswa pale anapotiwa nguvuni;


iii. kila mtuhumiwa ana haki ya kuelezwa kosa alilotenda kabla ya kukamatwa;


iv. kila mtuhumiwa ana haki ya kupewa ushauri wa kisheria;


v. Ana haki ya matibabu pale anapokuwa ameumizwa au anaumwa;


vi. Ana haki ya chakula na malazi;


vii. Ana haki ya kuwasiliana na ndugu zake;


viii. kila mtuhumiwa ana haki ya kukaa kimya mpaka pale anapo hitaji huduma ya kuwakilishwa;


ix. kila mtuhumiwa ana haki ya kupata dhamana isipokuwa kwa makosa yasiyokuwa na dhamana;

x. kila mtuhumiwa ana haki ya kuyafahamu mashitaka yake;


xi. Kila mtuhumuwa atachukuliwa kuwa mwenye akili timamu katika sheria ya makosa ya jinai hadi hapo itakapothibitishwa vinginevyo mbele ya sheria



MAMBO MACHACHE YANAYOWEZA KUKUONDOLEA JINAI MAHAKAMANI.

( a ) Kudai  haki  kwa  nia  njema, mtu  hatawajibika  na  kosa  la  jinai  kwa  kosa  linalohusiana  na  mali  iwapo  kitendo  kilichofanyika  au  kufanywa  na  huyo  mtu kilifanywa  kwa  nia  njema  ya  kudai  haki na  si  kwa  nia  ya  kuiba. 
Mfano  wa  hili  ni  kuwa  imetokea  kuna  mtu  unamdai  na  hataki  kukulipa, ukamzuia  na  kumnyaganya  mali  yake  iwe  gari, baiskeli , redio au  chochote,  basi  mtu  huyo  hawezi  kwenda  kufungua  kesi  ya  jinai  ya kumvamia,  au kumuibia.  Kifungu  hiki  kitakulinda  kwakuwa  umefanya  hivyo  kwa  nia  njema  ya  deni  lako  kwake. Kwahiyo  katika  hili  hautakuwa  na  jinai.

( b ) Kujilinda,kulinda  mtu  au  mali, mtu  hawezi  kuwajibika  kijinai  kwa  kitendo  alichokifanya  wakati  wa  kutimiza  haki  yake  ya  kujitetea/kujilinda, kumtetea mwingine,  kutetea  mali  yake  au  ya  mwingine.  Mfano  wa hili  ni  kuwa  imetokea   mtu  au  watu  wanataka  kukufanyia  fujo  kwa  namna  yoyote  ile.  Katika  kujitetea  wasikudhulu  ukamuumiza  au  hata  kumuua   mmoja.  Kwa  mazingira haya hautawajibika  kwa  jinai.  Au  umemkuta  mtu akiharibu  mali  yako  au  ya  mtu  mwingine. 

Katika  kumzuia  asifanye  hivyo  ukamuumiza  mtu  mwingine, ukaharibu  mali  nyingine    au  ukajikuta  umetenda  jinai  nyingine yoyote.  Basi hautawajibika  na  jinai  hiyo  kwakuwa  ulikuwa  ukilinda  mali  au  ukijitetea.

Muhimu  ni  kuwa  usitumie  nguvu  zaidi  kujitetea au  kujilinda  kuliko  nguvu  inayoshambulia. Kiwango  cha  kujilinda na  madhara  yaliyotokana  na  hilo  yasizidi   kiwango  cha  shambulio na  mazingira  yake  kwa  ujumla.

( c ) Dhania  isivyo  kweli mtu  ambaye  anatenda  kitendo  kwa  nia  njema  lakini  kwa  kukosea  kwa  kuamini  kuwepo  kwa  hali fulani  ambayo  kumbe  haipo  hatawajibika  kwa  kosa  la  jinai  kwa  kitendo  hicho. Mfano  wa  hili   ni  pale  ambapo  unaweza  ukampiga mtu katika  mazingira  ya kujihami usidhurike  ukidhani  ni  mwizi  lakini  baadae  unagundua  kuwa  hakuwa  mwizi.

Au  unamdhuru  mtu  kwa  kudhani  ni  mgoni  wako  kumbe  ni  mtu  mwema  aliamua  kumsaidia  mke  wako  baada  ya  kuzidiwa  ghafla. Ni  mazingira  kama  hayo  ambapo  utaondolewa  katika  jinai. Makala  nyingine  tutaangalia   matendo  mengine  yanayoweza  kukuondolea  jinai.
 UNAWEZA KUNIANDIKIA MAONI YAKO KUPITIA Dingadrizzy@ymail.com AU KWA KUCOMMENT AU KU SHARE NA WENGINE KAMA UMEIPENDA POST HII MTU WANGU

13 comments:

  1. Big up!!! Sanaaa brother! Kwa Kazi nzuriiiiiiiii

    ReplyDelete
  2. Tunashukuru sana ndugu kwa kutusaidia kwenye hili

    ReplyDelete
  3. Sheria inssemaje kama mimi nimfanyakazi wa mtu binafsi akawa hataki kunilipa ninapo mudai anasema tupige hesabu hesbu zinapingwa anakataa baazi ya fedha alizo chukuwa nakwambia zizitambui mfano hiyo hr imefumu zaidi ya miaka 4

    ReplyDelete
  4. somo n zur endeleleen kutufumbua macho

    ReplyDelete
  5. Asante kaka kwa kutupa ujumbe mzuri

    ReplyDelete
  6. Duuuh bro naomba unitafte kweny no hii Kuna ktu natak nkuulze unipe ushauri

    ReplyDelete
  7. Ahsante sana naomba unitafute nikuulize kitu au nikushirikishe kitu

    ReplyDelete
  8. Ahsante sana naomba unitafute nikuulize kitu au nikushirikishe kitu 0678732331

    ReplyDelete

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.