LONDONI: MEYA ATOA AGIZO UWANJA WA WEST HAM UCHUNGUZWE

Meya wa jiji la London Sadiq Khan
ameamuru kufanyika kwa uchunguzi juu ya ongezeko la gharama za Euro mil
50 wakati wa kuubadilisha uwanja wa West Ham.
Mwaka 2015,
aliyekuwa meya wa jiji hilo Boris Johnson alisema kuwa kubadilishwa
uwanja huo kutoka kuwa uwanja wa Olympic hadi kuwa uwanja wa mpira wa
miguu ungegharimu £ milioni 272, kiasi ambacho sasa kimepanda hadi
kufikia £ milioni 323.
Paul Fletcher ambaye amehusika katika ujenzi wa viwanja zaidi ya 30, anasema ni lazima uwanja huo ujengwe upya kutokana na majukwaa ya mashabiki kuwa mbali sana na uwanja jambo ambalo halipendezi kwa mchezo wa mpira wa miguu.
Leave a Comment