FAHAMU UTARATIBU WA UFUNGISHAJI NDOA

Image result for marriage photo black
NDOA NA NARATIBU ZAKE

TARATIBU ZA KUFUNGISHA NDOA
 
Sheria ya ndoa imeainisha utaratibu wa ufungishaji ndoa kuwa wa aina tatu;

• Ndoa za kiserikali: Hizi ni ndoa zinazofungwa bomani au kwa Mkuu wa Wilaya kwa
kufuata taratibu zilizowekwa na serikali.
• Ndoa za kidini: Ndoa zinazofungwa kwa kufuata taratibu zilizoainishwa na taasisi za
dini husika kama kanisa au msikiti.
Kumbuka
• Ndoa za kimila: Ndoa zinazofungwa kwa kufuata mila na desturi za kabila husika.
Ni muhimu ieleweke kwamba mwanamke hataruhusiwa kufunga ndoa nyingine
iwapo ndoa yake ya awali haijavunjwa kwa talaka ya mahakama.
Aidha mwanaume aliye katika ndoa ya mke mmoja hataruhusiwa kuoa mke mwingine.


Ni muhimu na ni utaratibu wa kisheria kusajili ndoa.
Ni muhimu kuwa na cheti cha usajili wa ndoa kwani ni utambulisho na uthibitisho wa
kuwepo ndoa halali.


 MAMBO YAPI UZINGATIUE KABLA UJAFUNGA NDOA? SOMA HAPA CHINI

• Kuwepo na muungano wa hiari kati ya mwanamke na mwanaume kabla ya kufunga
ndoa hufanya ndoa kuwa halali. Kifungu cha 16 cha Sheria ya Ndoa (marekebisho ya
mwaka 2002) vinazuia kuwepo kwa ulaghai au udanganyifu wa kati ya mwanamke
na mwanaume wanaotarajia kufunga ndoa.
• Muungano huo uwe unakusudiwa kuwa wa kudumu.
• Anayetaka kufunga ndoa asiwe katika ndoa nyingine. Hii ni kwa wale waliokwisha
kufunga ndoa ya mke mmoja au kama muumini wa dini ya kikristo na endapo ni
muumini wa dini ya kiislamu basi hataruhusiwa kuoa zaidi ya wake wanne. Kusiwe
na ndoa inayoendelea.
• Wafunga ndoa wasiwe watu walio na mahusiano ya karibu ya damu au kindugu
‘maharimu’. Sheria ya ndoa inazuia mtu kuoa au kuolewa na mzazi wake, baba au
mama wa kambo, mtoto au mjukuu, mtoto wa kufikia au kuasiliwa, kaka au dada,
shangazi au baba wa mjomba wake. (Kifungu 14 cha Sheria ya Ndoa).
• Wafunga ndoa wawe wametimiza umri unaokubalika kisheria ambao ni miaka 18 .
Chini ya umri huo iwapo tu kibali kimetolewa na wazazi kwa binti asiye chini ya miaka
15 na mahakama kwa asiye chini ya miaka 14. Mwanaume anaweza kuruhusiwa na
mahakama kuoa akiwa chini ya miaka 18 lakini si chini ya miaka 14 kama ataonyesha
kuelewa jukumu lake kama mtu mzima.
• Lazima ndoa inapofungwa wanaotarajia kufunga ndoa wawepo, Kutokuwepo kwa
wafungaji ndoa ni kinyume na sheria. Kwa mazingira Fulani hata hivyo sheria inaruhusu
ndoa kufungwa ikiwa mmoja wa wafunga ndoa hayupo lakini amewakilishwa na mtu
ambaye alikuwepo wakati mfunga ndoa ambaye hayupo, alipotoa ridhaa yake ya
kuoa au kuolewa.
• Pia mfugishaji ndoa lazima awe na leseni ya serikali inayompa mamlaka.a.
• Ndoa inapofungwa lazima ishuhudiwe na mashahidi wasiopungua wawili wenye umri
usiopungua miaka 18.


No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.