YOUNG D AFUNGUKA SABABU YA KUFANYA VIDEO NA TUNDA



Young Dee akiwa kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa
Radio alisema kuwa aliamua kufanya video hiyo na Tunda kwa sababu kwanza
ni mtu ambaye yupo naye karibu hivyo kwake haikuwa kazi ngumu kumuitaji
lakini pia adai alikutana na wanamitindo wengine ambao kwake walikuwa
wakubwa sana akamua ngoja afanye na mtu wake wa karibu.
"Kwanza unajua sijafanya muda mrefu video ya mapenzi, hivyo
nilifikiria nikaona Tunda ni mtu sahihi kwanza ni mtu wangu wa karibu
hivyo nikaona akisimama yeye kwenye video hii ataleta maana zaidi kwa
kile nilichokuwa nimelenga kukifikisha kwa jamii, maana nilikutana na
wanamitindo wengine kwangu walikuwa wakubwa sana. Lakini pia nikiwa na
Tunda muda wote kwangu ni furaha tu" alisema Young Dee.
Mbali na hilo anadai kuwa kipindi ambacho aliachia wimbo wake wa
'Hands up' ni kama alikuwa amewahi sana kwani alikuwa anajiona anahitaji
kupumzika kwanza, kujijenga upya ili kuingia kwenye ushindani kweli na
kufanya kazi rasmi.
"Kipindi kile kiukweli niliwahi sana maana tulikuwa na mizuka sana
lakini kuna siku nilipost picha Instagram mimi mwenyewe nilijiona
nimekonda kweli, nikaona nahitaji kupumzika, kulala vizuri na kufanya
mazoezi ili nikirudi nirudi kweli ndiyo kama sasa nipo fiti kwa
ushindani ndiyo maana nimekuja na hii kazi ya 'Furaha'" alisema Young
Dee
Leave a Comment