UCHAGUZI MKUU GAMBIA: UPINZANI WAONGOZA KWA KURA

 Adama Barrow ameshinda kwa kura nyingi mjini Banjul
Matokeo ya kwanza kutoka uchaguzi wa urais nchini Gambia yanampa mgombea wa upanzani Adama Barrow ushindi dhidi ya Rais Yahya Jammeh.
Mwandishi wa BBC nchini Gambia anasema amepata thibitisho kuwa bwana Barrow ameshinda kwenye mji mku Banjul.
Hata hivyo ni chini ya asilimia 15 ya karibu wapiga kura 890,000 waliosajiliwa ndio imehesabiwa.
Wanajeshi na polisi hii leo wameweka vituo vya ukaguzi kwenye barabara zinazoingia na kutoka mji mkuu.
Serikali ilizima huduma za mitandao na kufunga simu za kimataifa wakati uchaguzi ulikuwa ukiendelea.

Rais wa Gambia Jammeh

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.