TAARIFA RASMI KUTOKA JANGWANI: YANGA IMEMPIGA CHINI MBUYU TWITE
Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara Young Africans, wameamua
kuachana na Mbuyu Twite na nafasi yake kuchukuliwa na Justine Zulu.
“Justine Zulu ametafutwa baada ya kujua kwamba mkataba wa Mbuyu Twite
unaisha mwezi Disemba, Mkataba wa Twite umeisha na nafasi yake
imechukuliwa na Justine Zulu,” Baraka Deudedith akijibu kuhusu hatma ya
Mbuyu Twite ndani ya kikosi cha Yanga.
Ujio wa Zulu kwenye kikosi cha Yanga uliongeza idadi ya wachezaji wa
kigeni hadi kufikia nane (8) inyume na sheria na kanuni za ligi kuu
Tanzania bara ambapo vilabu husika vinapaswa kusajili wachezaji wa
kigeni wasiozidi saba (7).
Kwa hiyo moja kwa moja kanuni ziliitaka Yanga kupunguza mchezaji mmoja ambapo Mbuyu ikabidi apishe nafasi nafasi.
Kumekuwa na minong’ono kwamba huenda mchezaji huyo kiraka akajiunga
na Simba SC. Lakini jana uongozi wa Simba kupitia manager wake Musa
Hassan ‘Mgosi’ alikanusha taarifa za klabu yake kutaka kumsajili Mbuyu
Twite.


Leave a Comment