RAIS WA ANGOLA KUJIUZULU KABLA YA UCHAGUZI UJAO MWAKANI
Kituo cha radio cha Angola kinasema kwamba, Rais Jose Eduardo dos
Santos, ambaye ametawala taifa hilo kwa karibu miongo minne atajiuzulu
kabla ya Uchaguzi, mwaka ujao.
Waziri wa Ulinzi, Joao Lourenco, anatarajiwa kuwa mkuu wa chama kinachotawala cha MPLA.
Hii ni kumaanisha kuwa yeye atakuwa Rais iwapo chama chake kinashinda uchaguzi mwaka ujao.
Bwana
Dos Santos, ambaye ana umri wa miaka 74, wakati mmoja alikuwa kiongozi
mchanga zaidi katika Bara la Afrika aliposhinda uchaguzi wa kuwa Rais
akiwa na umri wa miaka 34 pekee.
Amewahi kusema kuwa hatashiriki uchaguzi lakini baadaye akabadilisha maoni yake na kusimama tena.
Makundi ya kupambana na ufisadi yamemlaumu kwa kuendesha serikali kama biashara ya kibinafsi


Leave a Comment