MSIBA MKUBWA INDIA: ALIYEKUWA MUIGIZAJI NA MKUU WA JIMBO LA TAMIL JAYALALITHAA JAYARAM, AFARIKI DUNIA

 Mwili wa Jayalalitha ukiwa umevikwa bendera ya India
Maelfu ya waombolezaji wamejitokeza kutoa heshima zao za mwisho kwa Jayalalithaa Jayaram, mmoja wa wanasiasa mashuhuri nchini India,.
Mkuu huyo wa serikali ya jimbo la Tamil Nadu alipatwa na mshtuko wa moyo Jumapili usiku na akafariki saa 23:30 (18:00 GMT) siku ya Jumatatu, kwa mujibu wa hospitali ya Apollo, mjini Chennai.
Mwili wake, ukiwa umevikwa bendera ya India, umewekwa kwa ajali ya kutazamwa na umma katika ukumbi mkubwa katika makao makuu ya jimbo hilo.

 Wafuasi wa Jayalalitha wakiwa na picha yake
Polisi wa ziada wametumwa kudhibiti waombolezaji na kushika doria huku kukiwa na wasiwasi wa kuzuka kwa fujo.
Alikuwa anaenziwa sana na wafuasi wake, baadhi ambao walikuwa wanamwita "Amma" (mama) na kuna wasiwasi kwamba huenda baadhi wakaamua kujidhuru au kuzua ghasia.


Awali, baada ya taarifa za kifo chake kutangazwa, kulitokea makabiliano kati ya polisi na wafuasi wake nje ya hospitali hiyo ya kibinafsi ya Apollo. Taarifa hizo baadaye ziliondolewa, ingawa saa chache baadaye alithibitishwa kufariki.
Jayalalitha aliishi maisha yenye visa vingi, hadharani na faraghani.
Aliigiza katika zaidi ya filamu 100 kabla ya kujiingiza katika siasa.
Jayalalitha baadaye alichukua udhibiti wa chama cha AIADMK kutoka kwa mke wa mwanzilishi wa chama hicho, na kisha akashinda uchaguzi 1991.
Alikuwa ametuhumiwa kwa kujihusisha na ufisadi, na alikaa jela vipindi viwili vifupi, karibuni zaidi 2014.
Mahakama kuu mjini Karnataka ilimuondolea makosa mwaka 2015 na akarejea uongozini.

 Maelfu ya watu wamejitokeza kutoa heshima za mwisho


No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.