KENYA: 30 NA ZAIDI WAFARIKI KWENYE MLIPUKO WA GARI AINA YA LORI


Idadi ya watu waliofariki katika ajali mbaya ya kuteketea kwa lori nchini Kenya, imepanda na kupata watu 30.
Kwa mjibu wa naibu kamanda mkuu wa jimbo la Nakuru Isaaca Masinde, ajali hiyo iliyotokea usiku wa kuamkia Jumapili katika eneo la Karai kwenye barabara ya kutoka Nairobi kuelekea Naivasha.
Lori moja la kubeba mafuta, lilianguka na kulipuka katika eneo la barabara hiyo yenye shughuli nyingi nchini Kenya na kusababisha mauaji ya watu 30 papo hapo.
Watu wengine zaidi wamefariki wakiwa kwenye matibabu mjini Naivasha.
Shirika la msalaba mwekundu nchini humo, limesema lori hilo la mafuta, lililokuwa njiani kuelekea nchi jirani la Uganda, lilipoteza usukani na kisha kugonga magari kadhaa kwenye barabara kati ya Nairobi na Naivasha yapata kimomita 100 kutoka mji mkuu Nairobi.

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.