ITAZAME LIST YA VILABU VILIVYOFANIKIWA KUFUZU HATUA YA 16 BORA LIGI YA MABINGWA ULAYA
Jumla ya timu kumi na sita zimefuzu
kwa hatua ya kumi na sita bora ya michuano ya klabu bingwa ulaya, huku
timu zilizomaliza katika nafasi ya tatu katika kila kundi zitaenda
kushiriki michuano ya Europa ligi.
Droo ya kupanga raundi ya
mtoano ya timu kumi na sita itapangwa siku ya jumatatu Decemba 12.Timu
zilizofuzu kutoa kundi A ni Arsenal wakiwa vinara wa kundi na pili
nafasi ya pili wako Psg, Kundi B vimefuzu timu za Napoli na Benfica.
Kundi
C wamefuzu vigogo Barcelona na Manchester City huku kundi D kukiwa na
Atletico Madrid na Bayern Munich.Kutoka kundi E zimefuzu Monaco na
Bayer Leverkusen, na kundi F wamefuzu Borussia Dortmund na Real
Madrid.
Leicester na Porto wamefuzu kutoa kundi G huku Juventus na Sevilla wakiwa wamefuzu katika kundi la mwisho kundi H


Leave a Comment