HALI YA CAZORLA BADO NI TETE, ATAKUWA NJE YA UWANJA KWA MIEZI MITATU
Kiungo wa kati wa Arsenal Santi
Cazorla, atafanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu, ambao utamfanya
kuwa nje ya uwanja kwa miezi mitatu.
Mchezaji huyo wa
kimataifa kutoka Uhispania, hajashiriki mechi yoyote tangu katikati mwa
mwezi Oktoba kutokana na jeraha hilo alilolipata walipokuwa
wakikabiliana na Ludogorets katika ligi ya klabu bingwa barani Ulaya.
Katika mechi hiyo Arsenal walitoka na ushindi mnono wa mabao 6-0 dhidi ya Ludogorets.
Arsenal wamesema tatizo linalomkabili Cazorla bado halijabadilika na atasafiri kuelekea Sweden wiki ijayo kwa upasuaji.
Cazorla, alikosa mechi saba msimu uliopita kutokana na jeraha la goti.
Amefunga magoli mawili katika mechi 11 zote alizoshiriki na klabu hiyo ya Gunners msimu huu.
Arsenal imesema,''upasuaji unahitajika kwa kifundo chake cha mguu wa kulia.''


Leave a Comment