FA YAWASHITAKI MAN CITY NA CHELSEA, ZITAZAME ADHABU ZILIZOTOLEWA
Klabu za Manchester City na Chelsea
zimeshtakiwa na FA kwa kushindwa kuwadhibiti wachezaji wakati wa mechi
ya Ligi ya Premia iliyochezwa Jumamosi.
Mashtaka hayo yanatokana
na vurugu za wachezaji zilizozuka dakika ya 95 wakati wa mechi hiyo
iliyochezewa Etihad ambapo Chelsea walishinda 3-1.
Mshambuliaji wa
City Sergio Aguero na kiungo wa kati Fernandinho walipewa kadi nyekundu,
lakini kiungo wa kati wa Chelsea Cesc Fabregas hakuchukuliwa hatua yoyote.
Meneja wa City Pep Guardiola aliomba radhi kwa mchango wa timu yake katika kisa hicho.
Aguero,
28, amepewa adhabu ya kutocheza mechi nne kutokana na makosa yake hii ikiwa ni mara ya pili kufukuzwa uwanjani kwa utovu wa nidhamu, baada ya
kumchezea visivyo beki wa Chelsea David Luiz.
Fernandinho walizozana na Fabregas baada ya tukio hilo la Aguero, na Mbrazil huyo atatumikia adhabu ya kukosa mechi tatu.
Klabu zote zimepewa hadi saa 18:00 GMT mnamo 8 Desemba kujibu mashtaka hayo.


Leave a Comment