AJALI YA NDEGE ILIYOIMALIZA TIMU YA CHAPECOENSE: MMOJA WA MCHEZAJI MAJERUHI KUWEZA KUCHEZA TENA
Neto
Mchezaji mmoja wa Brazil aliyesalimika katika ajali ya ndege huko nchini Colombia siku ya Jumatatu, anaweza akapona na kuweza kucheza tena.
Helio Hermito Zampier Neto mwenye miaka 31, beki wa Chapecoense alikuwa kwenye hali ya kawaida madokta wamesema baada ya kumfanyia upasuaji kwenye mguu, mapafu , mkono na kichwa.
Baba yake na Neto aitwaye Helam aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook,"Afya ya mwanangu inazidi kuimarika siku hadi siku, ameshafanyiwa upasuaji na madaktari wamesema anaweza kucheza tena soka... tuzidi kumuombea"
Watu watano walipona na 71 walipoteza maisha katika ajali ya ndege. Ndege hiyo ilikuwa ikiwasafirisha wachezaji wa Chapecoense na abiria wengine nchini Colombia. Timu ya uchunguzi ya Colombia wanasema ndege iliisha mafuta hivyo kuangukia milimani.
Rubani wa ndege hiyo Miguel Quiroga, alishapewa onyo la kutokuwa na mafuta katika ndege lakini alitupilia mbali ushauri huo, wameandika gazeti la Bolivian Deber
Heshima mbalimbali zimetolewa katika uwanja wa Chapecoense



Leave a Comment