ZAWADI ZA WASHINDI SASA ZAONGEZEKA KATIKA MASHINDANO YA CAF
Shirikisho la soka barani Afrika Caf
limeongeza kitita cha fedha zinazozawadiwa washindi katika michuano
yote kuanzia mwaka 2017 kueleka 2020.
Washindi wa kombe la mataifa
ya bara Afrika watapata dola milioni 4,wakati ambapo Ivory Coast
ilizawadiwa dola milioni 1.5 iliposhinda taji hilo mwaka 2015.
Mshindi
wa kombe la vilabu bingwa Afrika atajishindia dola milioni 2.5 badala
ya dola milioni 1.5 ambazo Mamelodi Sundowns walijishindia mwezi
uliopita.
Wakati huohuo fedha za mshindi wa kombe la mataifa ya bara Afrika
upande wa wanawake zitaongezwa na kufikia 80,000 mwaka 2019 kutoka dola
50,000 mwaka huu.
Fedha hizo ni chache mno ikilinganishwa na zile
inazopewa timu iliomaliza ya mwisho katika kombe la bara Afrika upande
wa wanaume.
Tizama hapa chini viwango vipya vya zawadi kwa washindi.



Leave a Comment