YAYA TOURE - "NILIJUA GUARDIOLA ATANIHITAJI TU"


Kiungo wa Manchester City Yaya Toure anasema hakushangaa kuitwa kwenye kikosi cha kwanza kilichovaana na Crystal Palace Selhurst Park.
Yaya Toure kwake ni mechi ya kwanza tangu kuwa kizuizini kwa miezi mitatu tangu msimu kuanza.
Yaya amesema," Nilijiandaa kimwili na kiakili kwani nilijua ipo siku kocha atanihitaji uwanjani, Nilipatwa na mshangao na kufurahi kupata nafasi ya kucheza. 
Wachezaji wenzangu ni watu muhimu sana, wamenipa support kwa kipindi chote hiki"
Yaya Toure aliingia matatani na kocha wake Pep Guardiola baada ya kuachwa nje kwenye kikosi kinachoshiriki Champions League msimu huu. Agent wake Seluk alidai huko ni kudhaluilishwa kwa mchezaji kama Yaya. Ambapo kwa kauli hizi Guardiola alidai bila kuombwa msamaha hatompa nafasi Yaya Toure ya kucheza tena.

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.