WIZKID AIRUDISHA TUZO YA MTV KWA MSHINDI HALALI AMBAYE NI ALI KIBA


Msanii alikiba anatarajiwa kupewa tuzo yake kutoka MTV EMA baada ya tuzo hiyo kupewa Wizkid kimakosa. 
Wizkid alipewa tuzo hiyo ya MTV EMA (MTV EUROPE MUSIC AWARDS) , wakati huo kwenye tovuti ya MTV ilionensha Ali kiba ndio anaongoza kwa kura.
Hali hiyo ilizua hali ya sitofahamu na malalamiko mengi kutoka kwa mashabiki wa mziki wa Ali Kiba. Baada ya malalamiko mengi msanii Ali kiba alipokea ujumbe kutoka MTV ukimjulisha kuwa yeye ndiye mshindi halali wa tuzo hiyo.
Tayari wizkid ameshafuta picha na taarifa zote zilizohusiana na tuzo hiyo huenda akawa kashapata taarifa tayari. Hata MTV nao wamezifuta post zao za kumpa ushindi wizkid.
Hongera alikiba hatimaye tuzo imerudi Tanzania.

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.