"VOTE FOR TRUMP"- UJUMBE ULIOANDIKWA BAADA YA KANISA LA WATU WEUSI KUCHOMWA MOTO MAREKANI NA WATU WASIOJULIKANA
Kanisa la watu weusi linalopatikana jimbo la marekani la mississippi limechomwa moto na watu wasiojulikana. Polisi katika jimbo hilo wanachunguza zaidi uhalifu huo wa hofu uliofanyika katika kanisa hilo linalotumiwa na watu weusi kwa kuteketezwa na moto na kuandikwa "Vote for Trump" ikiwa na maana ya "Mpigie kura Trump".
Hii inaweza kuwa kashfa mbaya kwa mgombea wa urais wa Republican Donald Trump, ikiwa tukio hili limetokea wiki moja tu mpaka kufikia siku ya uchaguzi utakaofanyika jumanne ijayo nchini marekani.
Msimamizi mmoja wa kituo cha zimamoto amedai kwamba kanisa hilo linaloitwa Hopewell Missionary Baptist Church, lilichomwa moto kwa makusudi. Kanisa hilo lilianzishwa miaka 111 iliyopita eneo la Greenville.
Maafisa wanasema ujumbe ulioandikwa kwenye jumba hilo ni wa kuzua hofu.
Meya
wa Greenville, Mississippi amesema kisa hitendo hicho ni cha "chuki na
woga" na shambulio la moja kwa moja dhidi ya uhuru wa watu kuabudu.
Kisa
hicho kinawakumbusha watu kuhusu visa vya kuchomwa moto kwa makanisa ya
watu weusi miaka ya 1950 na 1960, watu weusi waliokuwa wanapigania haki
zao.
Maafisa wa FBI wakishirikiana na wachunguzi wa jinai wa jimbo la Mississippi kwa sasa wanaendelea na uchunguzi.


Leave a Comment