VITA KUBWA INSTAGRAM: DIAMOND PLATNUMZ NA OMMY DIMPOZ WARUSHIANA MANENO YA SHOMBO

Katika hali ya kawaida ni kitu kisichoshangaza ukiona watu waliokuwa marafiki wakubwa wakigombana lakini hili halikutarajiwa kwa hawa waliokuwa maswahiba wakubwa Ommy Dimpoz na Diamond Platnumz kama watafkia huku. 


Rich mavoko na Diamond wameweka utani katika ngoma yao mpya juu ya ishu ya Ali kiba kuzimiwa mic katika Tamasha lililofanyika Mombasa, na Diamond akaandika kwenye mtandao wa instagram,"Kushindana na Wasio Jua Raha sana hahahahahaham #Hawatoweza,
Ommy Dimpoz nae akajibu mapigo kwa kuandika hivi
Wazee Wa Kupanik Mbona Kama Povuuu Linawatoka 😂😂#TeamMzikiMzuri VS #TeamUjanjaUjanja
#Kajiandae
#KabaliYao
#WeDontBuyViews
#MeNilijuaTunafanyaMzikiKumbeVitaaa🙌😂
#NawajuaWazeeWaKuchambaNataniaTu😂
#PiaNawajuaKwaMitusiLakiniNishajiandaa😂😂
#NawaachiaUwanjaMweupeeeWalaSiblokuMtu
#NachangamshaBarazaKidogoooo😂
Ommy Dimpoz aliwahi kunukuliwa kwenye kituo kimoja cha radio kwamba wasanii wananunua viewers kwenye Youtube ili video yake ionekane imetizamwa na watu wengi zaidi.
Diamond nae hakuishia hapo aliongezea dongo lingine akasema," “Mtoto wa Kiume kumchukia Mwanaume Mwenzio kisa Kakataa kukupumulia nayo ni #KOKORO.”
Ni kipindi kirefu sana mastaa hawa wawili waliokuwa marafiki wakubwa hawaelewani na hawana uhusiano mzuri.

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.