UNA UWEZO WA KUCHEZEA MPIRA (FREESTYLE)? IANGALIE HAPA FURSA HII YA MSHINDANO YA FREESTYLE FOOTBALL TANZANIA
Jacob Mbuya mratibu wa mashindano hayo
Freestyle Football Tanzania kwa kushirikiana na kipindi cha Sports
Bar cha Clouds TV wamezindua rasmi sindano la kumtafuta bingwa wa
kuchezea mpira wa miguu kwa mkoa wa Dar es Salaam.
Mchakato wa kumpata bingwa wa Freestyle Football utafanyika katika
wilaya tatu za Dar es Salaam (Temeke, Ilala na Kinondoni) kisha fainali
itafanyikia Coco Beach.
Temeke itakuwa wilaya ya kwanza ambapo washindi watano watatafutwa
tarehe 19 November kwenye uwanja wa Mwembe Yanga, ikifuatiwa na Ilala
November 26 kisha Kinondoni watahitimisha Disemba 3 kabla ya fainali
inayotarajiwa kufanyika Disemba 11 mwaka huu.
“Malengo ya shindano hili ni kuibua vipaji na kutoa fursa kwa vijana.
Tumeanza na mkoa wa Dar es Slaam, panapo majaaliwa tunatarajia tufanye
shindano hili kwenye mikoa mingine ili kupata bingwa atakaye tuwakilisha
katika mashindano ya kimataifa,” amesema Mwenyekiti wa kamati ya
mashindano Bw. Pascal Chang’a.
Amewaomba wadau wajitokeze kwa wingi katika shindano hilo
linalodhaminiwa na RedBull na kuratibiwa na Shadaka Sports Management,
vilevile amefungua milango kwa kampuni nyingine kujitokeza kudhamini
shindano hilo ambalo lina malengo chanya kwa jamii.


Leave a Comment