UGANDA : MAAFISA WAFUNGWA MIAKA 10 JELA KILA MMOJA KWA UBADHILIFU WA PESA ZA MFUKO WA UZEENI
Maafisa watatu wa vyeo vya juu
nchini Uganda wame hukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani kwa ufujaji wa
karibu Dola milioni ishirini na tano,kutoka hazina ya malipo ya uzeeni.
Mahakama moja mjini Kampala imewapata maafisa hao na makosa ya
kuelekeza malipo ya uzeeni ya zaidi ya watu elfu mbili, katika akaunti
zao za kibinafsi.
Mahakama hiyo aidha imesema watatu hao wanaweza
kukata rufaa dhidi ya huku hiyo. Maafisa wengine watano wa vyeo vya
chini katika hazina hiyo ya uzeeni, pia wanatarajiwa kushtakiwa wa
makosa sawia na hayo.


Leave a Comment