TRUMP - "NINAHITAJI KULIPWA DOLA MOJA TU KWA MWAKA KAMA MSHAHARA WANGU WA URAIS"
Rais mteule wa Marekani Donald Trump
amesema hataki kulipwa mshahara wa rais wa $400,000 atakapochukua kijiti cha urais Januari mwakani. Badala yake atakuwa akilipwa $1 pekee kila
mwaka.
Alifichua mpango wake huo wakati wa mahojiano na Lesley Stahl kipindi cha 60 Minutes cha CBS News.
Ingawa hakujua rais huwa analipwa pesa ngapi, Bw Trump alisema alidhani anahitaji kuchukua tu $1.
Baada ya Bi Stahl kumjulisha kwamba mshahara wa rais ni $400,000, alisema: "Hapana, sitaupokea mshahara huo. Sizichukui kamwe."
Donald Trump anatimiza ahadi zake alizoahidi katika kampeni zake kwamba hatochukua mshahara wake kwani sio jambo kubwa kwake bali maslahi ya wananchi wa marekani.
Donald Trump sio kiongozi wa kwanza kukataa mshahara, soma hapa orodha ya viongozi waliowahi kukataa mishahara yao.
Herbert Hoover, aliyekuwa ametajirika kupitia biashara ya madini kabla
ya kuingia madarakani, na John F Kennedy, aliyerithi utajiri wote
walikataa kupokea mashahara na badala yake wakatoa pesa hizo zisaidie
wasiojiweza katika jamii.
Rais aliyetawala marekani karne ya 20, John F Kennedy
Meya wa zamani Michael Bloomberg, gavana wa zamani wa California
Arnold Schwarzenegger na gavana wa zamani wa Massachusetts Mitt Romney
pia walikataa kupokea mishahara yao.
Mark Zuckerberg, mwanzilishi
wa mtandao wa kijamii wa Facebook, ndiye mfanyakazi anayelipwa mshahara
wa chini zaidi katika kampuni hiyo.
Aidha, ni miongoni wa CEO (Afisa Mkuu Mtendaji) wengi ambao hulipwa mshahara wa $1 pekee.
Sergey Brin na Larry Page wa Google pia wamekuwa wakilipwa $1 kwa mwongo mmoja sasa.
Wazo la kulipwa dola moja lililetwa na mwanzilishi wa bidhaa za apple Steve Jobs aliporejea katika shirika la Silicon Valley mwaka 1997.
Steve Jobs
Hata hivyo Donald Trump ana biashara zake zinazomuingizia pesa nyingi hivyo utajiri alio nao hautaingia dosari kwa kukosa mshahara wake wa urais.




Leave a Comment