TRUMP KUZIFUTA SERA ZOTE ZA OBAMA ZENYE UHUSIANO NA CUBA
Rais mteule wa Marekani, Donald
Trump, ametishia kufutilia mbali sera ya rais Barrack Obama ya kurejesha
uhusiano kati ya Marekani na Cuba wakati atakapochukua madaraka Januari
mwakani.
Trump amesema uamuzi huo utategemea utawala wa
kikomyunisti mjini Havana, kuweka sera ambazo zitaimarisha hali ya
maisha kwa raia wa nchi hiyo, na wale waliochukua uraia wa Marekani na
wale wa Marekani.
Utawala wa rais Obama umejitahidi kurejesha uhusiano na utawala wa Havana, baada ya uhasama uliodumu kwa zaidi ya miaka hamsini.
Trump amemtaja marehemu Castro kama kiongozi mkatili wa kiimla ambaye aliwakandamiza raia wake kwa miongo kadhaa
Leave a Comment