TRUMP ASEMA HATOIONDOA BIMA YA AFYA YA OBAMA KAMA ALIVYODAI KATIKA SERA ZAKE
Rais mteule wa Marekani Donald Trump
aliyefanya kampeini ya kupinga Bima ya afya inayofaahamika kama Obama
care, sasa amesema atafanyia marekebisho machache kipengee cha sheria
juu ya bima hiyo ya matibabu kwa gharama nafuu.
Katika mahojiano
ya kwanza tangu achaguliwe rais siku ya Jumanne, Trump ametangaza
mageuzi makubwa ya sera punde atakapochukua nafasi ya Barack Obama
katika Ikulu ya White House mwezi Januari mwaka ujao.
Bwana Trump,
aliyesisitiza vikali kuwa atafutilia mbali bima hiyo inayowapa fursa
mamilioni ya Wamarekani maskini kupata huduma ya afya kwa bei nafuu
punde tu atakapochaguliwa rais, yaonekana amebadilisha msimamo wake juu
ya suala hilo.
Na Katika kile kinachoonekana kulegeza msimamo wake
juu ya mpinzani wake Hillary Clinton, Rais huyo mteule amesema,Clinton
ni mwanamke mkakamavu na mwenye tajiriba kubwa.


Leave a Comment