TRUMP AANZA KAZI YA UTEUZI WA AWALI
Donald Trump akiwa na Reince Pribeus
Rais mteule wa Marekani, Donald
Trump, amemteua mwenyekiti wa kamati ya taifa ya chama cha Republican,
Reince Priebus, kutumika kama mkuu wa wafanyakazi.
Bwana Priebus
ana uhusiano wa karibu na spika wa baraza la wawakilishi Paul Ryan.
Wandishi wa wa habari wanaarifu kwamba uteuzi wa Piebus unaweza kuwaudhi
wafuasi wake wa hali ya chini na hii inaashiria kwamba uongozi ujao
unalenga kufanya kazi kwa karibu na baraza la Congress kujihakikishia
ushindi wa mapema wa baraza hilo.
Stephen Bannon, alikuwa ni mwenyekiti wa taasisi ya Breitbart News,
ambayo ni tovuti yenye maoni ya mrengo wa kulia , naye ameteuliwa kwa
nafasi ya mkuu wa mipango na mshauri mwandamizi.
Stephen Bannon
Mkuu wa
wafanyakazi ambaye anafanya kazi kama mruhusu na mtengeneza ajenda kwa
rais, na kwamba ni mmoja wa chaguo muhimu la mapema kwa rais ajae.
Katika
taarifa yake, Trump alinukuliwa akiwazungumiza Priebus na Bannon ni
viongozi wenye sifa za hali ya juu waliofanya kazi pamoja wakati wa
kampeni zake za kuingia Ikulu ya Marekani.
Leave a Comment