TP MAZEMBE MABINGWA WA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA
Wachezaji wa TP mazembe wakishangilia kutwaa ubingwa
Timu ya TP Mazembe ya Congo imetwaa
ubingwa wa kombe la shirikisho barani Africa, baada ya kuichapa Mo
Bejaia ya Algeria kwa 4-1 katika mchezo wa fainali ya pili.
Mabao mawili ya kiungo Rainford Kalaba na mengine ya Merveille Bope na Jonathan Bolingi yametosha kuipa TP Mazembe Ubingwa.
Sofiane
Khadir aliifungia timu ya Algeria bao la kufutia machozi na kufanya
matokeo ya jumla yawe 5-2 baada ya sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza
wiki iliyopita mjini Blida.
Mazembe sasa watamenyana na washindi
wa Ligi ya Mabingwa, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kati ya Februari
17 na 19 mwakani kuwania taji la Super Cup ya CAF.
CHANZO: BBC Swahili


Leave a Comment