TANZIA: GOLIKIPA WA TIMU YA TAIFA YA WANAWAKE YA GAMBIA AMEFARIKI DUNIA AKIJARIBU KUZAMIA ULAYA KUPITIA BAHARI YA MEDITERRANIA

Katika hali ya kwenda kutafuta maisha yanayoaminika kuwa bora barani ulaya, waafrika wengi huzamia kwenda barani ulaya kwa njia ya bahari kutumia majahazi au boti ndogo. 
Wahamiaji 239 wanaaminika kufa maji katika ajali iliyohusisha kuzama kwa boti mbili zilizokuwa zikijaribu kuvuka bahari ya mediterrania kuingia nchini Italy.
Katika ajali hiyo mmoja wa wahanga ni golikipa wa timu ya taifa ya Gambia ya wanawake mwenye miaka 19, Fatim Jawara. Familia yake imethibitisha kifo chake kupitia Taasisi ya kusimamia mpira ya Gambia.
Fatim Jawara alianza kuitumikia timu ya taifa mwaka mmoja uliopita baada ya kuonesha uwezo kwenye timu ya watoto.


"Atakumbukwa sana kwa kuokoa mkwaju wa penalty katika moja ya mechi zake za kirafiki dhidi ya Scotland"  anasema Mr Bajo alipokuwa akizungumza na shirika la utangazaji la AFP.
Zaidi ya wahamiaji 4200 hupotea au kufa maji wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterrania kuingia ulaya, takwimu hizi zimetolewa na International Organization for Migration (IOM).

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.