TANZANIA SASA YAPATA MADINI MAPYA YALIYOGUNDULIWA MERELANI

Katika kile kinachosemekana kwa Tanzania kusheheni rasilimali nyingi za kuipa Nchi utajiri sasa imethibitika. Madini mapya aina ya Merelaniite yamegunduliwa huko Manyara katika milima ya Lelatema wilaya ya Simanjiro, jina hilo limetokana na eneo lenyewe madini hayo yalipogunduliwa hapo Merelani (Merelaniite) na eneo hilo linasifika sana kwa upatikanaji wa madini aina ya Tanzanite.

 Madini aina ya Merelaniite yaliyogunduliwa Manyara
Madini hayo yaligunduliwa na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Kiteknolojia cha Michigan cha Marekani, makavazi ya historia asilia ya London, chuo kikuu cha Di Firenze cha Italia na makavazi ya historia asilia ya Smithsonian ya Washington.
Wataalamu sita waliofanya uchunguzi, kwenye makala iliyochapishwa kwenye jarida la Minerals (Madini) wanasema madini hayo yana vipande vinavyofanana na sharubu vya rangi ya kijivu vya urefu wa milimita moja hivi, ingawa kuna baadhi vyenye urefu wa hadi mililita 12.
"Madini haya mapya yametambuliwa na taasisi inayoyapa majina madini, IMA CNMNC (2016-042), na kupewa jina linalotokana na eneo yalipogunduliwa kwa heshima ya wachimba migodi wa eneo hilo wa zamani, wanaoishi na wanaofanya kazi," makala ya wataalamu hayo inasema.

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.