"SIWEZI KUMUOMBA MSAMAHA PEP GUARDIOLA" - WAKALA WA YAYA TOURE AMEYASEMA HAYA

Wakala wa star wa soka wa Manchester cty na Ivory Coast, Dimitri Seluk amegoma kumomba radhi Pep Guardiola.
Kauli hiyo imefuatiwa baada ya kiungo wa Manchester City Yaya Toure, kuomba radhi kupitia mitandao ya kijamii kwa uongozi wa timu yake. Muda mfupi baada ya Yaya Toure kuomba radhi, wakala huyo alijiunga mara moja na Alan Brazil Sports Breakfast .
Baada ya hapo wakala huyo raia wa Ukraine alisema alikuwa na shauku ya kujenga amani baina yake na kocha wa Man city Pep Guardiola lakini sio kumuomba radhi.

 Wakala Dimitri Seluk akiwa na Yaya Toure
"Kuomba msamaha? kwa nini niombe msamaha?, nilitaka kuweka mambo sawa baina yangu na Pep lakini sio kumuomba msamaha. Wachezaji mahiri na wanaokula mishahara mikubwa kama Yaya Toure hawatakiwi kukaa bench, inabidi wachezeshwe" alisema wakala wa Yaya, Dimitri Seluk.
Hata hivyo wakala huyo amedai Yaya ana mengi ya kuonesha ndani ya uwanja pindi atakaporejea katika kabumbu iwapo atapewa nafasi na kocha wake.
Sekeseke hili lilitokea baada ya kocha Pep Guardiola kumuacha Yaya Toure katika kikosi cha wachezaji watakaoshiriki champions league. Dimitri Seluk hakufurahishwa na hili hivyo akaamua kutangaza kwenye media kwamba Pep ni kocha asiyethamini wachezaji wakubwa kama Yaya Toure, baada ya kauli hii Guardiola alinukuliwa akisema hatomchezesha tena Yaya Toure mpaka pale atakapoomba radhi. 

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.