RAIS WA URUSI PUTIN AAHIDI KUBORESHA UHUSIANO NA RAIS WA MAREKANI DONALD TRUMP
Raisi wa Urus Vladimir Putin amesema kuwa Rais mteule wa Marekani Donald Trump ameridhia kuungana na mataifa yenye nguvu.
Putin
amesema yuko tayari kurudisha mahusiano yao yaliyokuwa yanaenda mrama
kutokana na mzozo wa Ukraine na Syria ingawa tarehe ya kukutana kwao
haijatajwa bado.
kiongozi huyo wa Urusi pia amesema kuwa kulikuwa na tofauti kubwa kati ya sera na kampeni za kisiasa za Marekani.
Rais
huyo mteule wa Marekani anaendelea kukutana wanachama muhimu wa bunge
na mojawapo ya watu anaotazamia ni Jenerali James Mattis anayejulikana
kwa kikosi chake kama mbwa mwenye hasira ambaye ni mgombea anayeongoza
katika kinyanganyiro cha kuwa waziri wa ulinzi wa marekani.
Kumekuwa
na tetesi kuwa trump atamteua aliyekuwa mgombea wa Urais Mitty Romney
katika ngazi ya juu ya uongozi, aliyewahi kusema kuwa Trump ni laghai.


Leave a Comment