RAIS MOSRI ALIYEPINDULIWA MISRI AFUTIWA HUKUMU YA KIFO


Mahakama nchini Misri imebatilisha hukumu ya kifo aliyopewa rais aliyepinduliwa Mohammed Morsi.
Morsi alihukumiwa kifo baada ya kulaumiwa kuhusika na kutoroka kwa wafungwa wengi wakati wa mapinduzi ya mwaka 2011.
Alichaguliwa kuwa rais mwaka 2012 lakini akaondolewa na jeshi mwaka mmoja baadaye, kufuatia maandamano makubwa ya kupinga utawala wake.
Morsi ashahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa mashtaka yanayohusu ugaidi na bado anakabiliwa na mashtaka kwa makosa mengine

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.