RAIS MAGUFULI ASAINI MSWADA WA SHERIA YA WANAHABARI
Rais wa wa Tanzania John Pombe
Magufuli ametia saini Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 ambayo
imekuwa ikipingwa na wadau katika sekta ya uanahabari nchini humo.
Sheria hiyo iliyopitishwa na Bunge la Tanzania Jumamosi 5 Novemba mjini Dodoma.
Taarifa
kutoka kurugenzi ya mawasiliano ya rais imesema Rais Magufuli alitia
saini Sheria hiyo tarehe 16 Novemba na kwamba anaamini sheria hiyo
itakuwa na manufaa mengi.
"Naamini kuwa Sheria hii itasaidia
kuboresha sekta ya habari kwa manufaa ya wanataaluma wenyewe na Taifa,"
amesema Rais Magufuli.


Leave a Comment