PICHA : AJALI YA TRENI YAUA MAMIA YA WATU NCHINI INDIA

Idadi ya watu waliyofariki kutokana na ajali ya treni iliyotokea mapema leo kaskazini mwa India, imeongezeka hadi tisini na tisa na kuwajeruhi mamia ya wengine.
Treni hiyo ilikuwa ikitoka Indore kuelekea Patna kabla ya kupoteza muelekeo na kutoka katika barabara ya reli na kuanguka ilipokaribia mji wa Mashariki wa Kanpur katika jimbo la Utter Pradesh.
Maafisa wa kutoa huduma za dharura wanajaribu kuwaokoa manusura waliokwama katika mabehewa yaliyoanguka.
Waziri wa uchukuzi wa India ameamuru kufanywa kwa uchunguzi kubaini kilichosababisha ajali hiyo
 Nimekuwekea hapa picha za ajali hiyo.




No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.