OBAMA NA TRUMP USO KWA USO WHITE HOUSE LEO HII
Rais mteule wa Marekani Donald Trump anajianda kuelekea Ikulu ya
White House kuanza mazungumzo na Rais Barack Obama, kuhusu kupokezana
madaraka. Trump ataandamana na mkewe Melania ambaye atakutana na
michelle Obama.
Licha ya tofauti zao, bwana Obama siku ya Jumatano
aliishauri timu yake kufanya jitihada zaidi kuhakisha kuwa kuna
mafanikio kwenye shughuli ya kupokeza madaraka kwa Republican mwezi
Januari.
Mapema timu ya kampeni ya Trump ilikutana na washauri
kujadili masuala kuhusu siku za kwanza 100 za Trump kama rais na uteuzi
muhimu katika nyadhifa za serikali.
Majina yaliyotajwa ni kati ya
wale waliomuunga mkono Trump kutoka mwanzo akiwemo aliyekuwa spika Newt
Gingrich, maseneta Jeff Sessions na Bob Corker pamoja na aliyekuwa meya
wa New York Rudy Giuliani.
Leave a Comment