NJAA KALI YAITAFUNA NIGERIA
Umoja wa Mataifa umetoa tamko kwamba
wanaijeria wapatao nilioni kumi na nne wanahitaji misaada ya
kibinadamu upande wa Kaskazini mwa nchi hiyo, mahali ambako maelfu kwa
mamia ya watoto wako kwenye hatari kubwa ya kifo kutokana na njaa kali
na kwamba watoto laki nne wanahitaji msaada wa dharula.
Inaelezwa
kuwa mkoa uliokumbwa na baa hilo la njaa awali ilikuwa ngome ya zamani
ya kundi la dola ya kiislamu Kiislam, Boko Haram.Jimbo hilo lilikuwa
katika hali tete kiasi cha kutokufikiwa na misaada ya kibinaadamu kwa
miaka kadhaa sasa ambapo kwa sasa ndiyo limebainika kuwa na hali mbaya
ya chakula na njaa kali ikiwemo majimbo ya Borno,Yobe na Adamawa.
Shirika
la kuwasaidia watoto la , Unicef, limesema kwamba inakadiwa kuwa
watoto wapatao elfu sabini na watano wako katika hatari ya kufa.
Mapema
, shirika la misaada ya kitabibu la madaktari wasio kuwa na mipaka
wamegundua idadi kubwa zaidi ya watoto walio chini ya umri wa miaka
mitano katika kambi mbili za wakimbizi utafiti ambao uliainishwa kwa
kiasi kikubwa kuwa wa chini kuliko ilivyotarajiwa, na kwamba inaaminika
robo ya watoto hao walikwisha kufa .


Leave a Comment