"NITAKUWA RAISI WA WAMAREKANI WOTE" - ISOME HAPA HOTUBA YA TRUMP BAADA YA KUSHINDA URAIS

 Trump baada ya kushinda urais Marekani
 
Donald Trump ameshinda kiti cha urais mapema asubuhi ya leo baada ya kumshinda mpinzani wake Hilary 
Clinton. Rais huyo kutoka chama cha Republican ameshinda kwa kura nyingi katika majimbo ya Florida, North Carolina na Ohio.
Baada ya ushindi huo, Donald Trump ametoa hotuba fupi hivi punde na haya ndio aliyoyasema:-
"Nitawafikia wale wote walioniunga mkono na ambao hawakuniunga mkono, ni muda wa kutibu vidonda vya utengano nawaambia wote Republican na Democratic tuwe na umoja.
Nitakuwa raisi wa wamarekani wote, waume kwa wanawake waliosahaulika katika taifa hili hawatasahaulika tena. Kwangu hii haikuwa kampeni bali harakati zilizonifanya niingie white house.Ushindi huu haukuwa rahisi, ni kazi kubwa naishukuru sana familia yangu kwa kuwa pamoja nami".
Mr Trump pia hakuacha kumsifia mpinzani wake Hilary Clinton na kudai kuwa angependa kushirikiana nae katika kuijenga nchi ya Marekani, ambapo katika hili watu wengi walipiga makofi ya heshima kwa tukio hili.
Mr Trump aliendelea kusema,"Tutaungana na mataifa ambayo yangependa kuungana nasi, tutafanya kazi kwa haki, tutapenda kufikia muafaka unaotufaidisha sote sio ugomvi na mifarakano. Marekani isitarajie chochote zaidi ya vitu bora, lazima tujue na tudai muafaka wetu.
Rais Donald Trump alimaliza hotuba yake kwa kusema, "Naipenda hii Nchi".

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.