NDEGE ILIYOBEBA WACHEZAJI WA KLABU YA NCHINI BRAZIL YAANGUKA COLOMBIA

 Mabaki ya ndege hiyo baada ya ajali
Ndege iliyobeba watu 81, wakiwemo wachezaji wa klabu moja ya soka ya Brazil, imeanguka eneo la Medellin nchini Colombia.
Taarifa zinasema watu 25 wamethibitishwa kufariki na sita wamenusurika..
Ndege hiyo inadaiwa kupata hitilafu za mfumo wake wa umeme.
Ndege hiyo ilikuwa safariki kutoka Bolivia na ilikuwa imewabeba wachezaji wa timu ya Chapecoense, ambao walikuwa wamepangiwa kucheza mechi ya fainali ya Copa Sudamericana, dhidi ya timu ya Medellin, Atletico Nacional.

 wachezaji wa Chapecoense katika moja ya mechi zao
Mechi ya awamu ya kwanza ya kombe hilo, la pili kwa umuhimu Amerika Kusini, ilikuwa imepangiwa kuchezwa Jumatano lakini sasa imesitishwa.
Timu hito inayotoka mji wa Chapeco, kusini mwa Brazil, ilipandishwa kucheza ligi ya daraja ya kwanza nchini Brazil mwaka 2014 na ilifika fainali ya kombe hilo la Sudamericana kwa kulaza San Lorenzo ya Argentina.
Taarifa zinasema ndege hiyo muundo wa British Aerospace 146 ambayo imekuwa ikitumiwa na shirika la ndege la Lamia la Bolivia ilikuwa na abiria 72 na wahudumu tisa.
Maafisa wa klabu hiyo ya Chapecoense wametoa taarifa wakisema: "Tunamuomba Mungu awe na wachezaji, maafisa, wanahabari na wageni wengine watu ambao walikuwa wameandamana na ujumbe wetu."

 kikosi cha waokoaji kikisogea eneo la tukio
Wamesema hawatatoa taarifa nyingine hadi ibainike kiwango kamili cha mkasa huo.
Taarifa zinasema watu wawili kutoka kwa timu hiyo - Alan Ruschel na Danilo - huenda wamenusurika.
Telemundo Deportes wameandika kwenye Twitter kwamba Ruschel ameathiriwa na mshtuko lakini ana fahamu na anazungumza. Aidha, ameomba aruhusiwe kukaa na pete yake ya harusi na awaombe jamaa zake.

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.