MWONGOZO NA MATUKIO MBALI MBALI YA UCHAGUZI MAREKANI
Wamarekani wanapiga kura kuamua atakayekuwa rais wao wa 45. Hapa ni mambo muhimu ya kufuatilia wakati wa uchaguzi.
Majimbo
yote 50 pamoja na Washington DC (eneo ambalo halijatambuliwa kama
jimbo) watapiga kura katika nyakati sita tofauti za uchaguzi.
Tofauti
hii inatokana na ukubwa wa taifa hilo, ambapo majimbo yaliyo mashariki
yatatangulia kupiga kura na yale yaliyo magharibi yatakuwa ya mwisho.
Lakini kinyume na demokrasia nyingi, anayeshinda kura nyingi kitaifa si lazima awe ndiye atakayeibuka mshindi.
Marekani huwa na mfumo tofauti wa uchaguzi ambapo mshindi anahitajika kushinda kura 270 za wajumbe kati ya 538 zinazoshindaniwa.
Maeneo
mengi Marekani yatasubiri vituo vifungwe- sana kati ya 19:00 EST (24:00
GMT) na 20:00 EST (01:00 GMT) - kuanza kupokea matokeo na makadirio ya
matokeo katika majimbo mbalimbali.
Hata hivyo, kijiji kimoja kwa
jina Dixville Notch katika jimbo la New Hampshire, kina desturi ya
kupiga kura usiku wa manane. Kijiji hicho kitakuwa kimetangaza matokeo
yake hata kabla ya upigaji kura kumalizika katika maeneo mengine. Hilo
litakuwa mwendo wa saa 00:01 EST (05:01 GMT).
Hapa ni baadhi ya
mambo ambayo huenda yakatokea, kwa kutegemea wakati ambao vituo vya kura
vitafungwa. Hata hivyo, kuna uwezekano wa kuwepo tofauti kidogo katika
wakati wa kufungwa kwa matokeo.
BBC itakuwa inategemea makadirio
ya mshirika wake Marekani, ABC, kwa sababu inaweza ikachukua siku kadha
kabla ya kura zote kuhesabiwa.
Na kuhusu matokeo kamili? Kaa
chonjo na simu yako au uwe macho kwenye runinga mwendo wa saa 23:00 EST
(04:00 GMT). Ukiona huenda ukapitwa kwa sababu ya usingizi, unaweza
kuweka kengele ya saa ya kukuamsha. Huo ndio wakati upigaji kura
utamalizika pwani ya Magharibi mwa Marekani. Historia inaonesha huo ndio
wakati mshindi hutangazwa. Ilikuwa kabisa wakati huo ambapo mshindi
alijulikana mwaka 2008, na dakika 15 baadaye mwaka 2012
Vituo vya kura Pwani ya Mashariki vyafungwa na kuhesabiwa kwa kura kuanza.
Macho ya wengi yatakuwa jimbo la kushindaniwa la Virginia (kura 13 za wajumbe), ambalo lilimpigia kura Barack Obama mwaka 2008 na 2012 lakini awali lilikuwa la Republican.
Donald
Trump akishinda huko, au amkaribie sana Hillary Clinton, itakuwa ishara
kwamba huenda ukawa usiku mrefu kwa wafuasi wa Democratic, kwa mujibu
wa mwandishi wa BBC Amerika Kaskazini Anthony Zurcher.
Jimbo la Georgia (16)
pia ni muhimu. Jimbo hilo limeunga mkono chama cha Republican tangu
1996, lakini ubabe wa chama hicho umekuwa ukipungua miaka ya karibuni.
Pia, kunatarajiwa makadirio ya matokeo kutoka jimbo la Indiana (11), nyumbani kwa mgombea mwenza wa Trump Mike Pence, Kentucky (8), South Carolina (9) na Vermont (3)
akadirio ya matokeo Virginia Magharibi (5), jimbo ambalo limeunga mkono Republican tangu 2000.
CHANZO CHA HABARI : BBC Swahili



Leave a Comment