MWATHIRIKA WA UKIMWI ASHTAKIWA KWA KUFANYA MAPENZI NA WANAWAKE 104 MALAWI
Uamuzi wa kesi ya mwanamme mmoja
nchini Malawi unatarajiwa kutolewa wiki hii, baada ya kuiambia BBC kuwa
alifanya mapenzi na wasichana kama sehemu ya mila.
Eric Aniva
alikamatwa mwezi Julai kufuatia amri ya rais, baada ya kukiri kuwa
alifanya mapenzi yasiyo na kinga na wasichana walio na umri wa hadi
miaka 12, na kuwa kimya juu ya hali yake ya kuugua ugonjwa wa ukimwi.
Mshtakiwa mwathirika Eric Aniva
Aniva
anasema kuwa alipewa vibarua na familia za wasichana hao kushiriki
mapenzi nao, kwa tamaduni ambayo jamii inaamini kuwa huwezesha wasicha
kuingia utu uzima.
"Tunaamini kuwa ikiwa mjane au mwanamme
aliyefiwa hawezi kusafishwa kwa njia ya mapenzi, huenda kisa kibaya
kikafuatia kama kifo kwa majane au mwanamme aliyefiwa au kwa ukoo
mzima," alisema mhudumu mmoja wa jamii.
Wakati rais wa Malawi Peter Mutharia aliamrisha mwanamme huyo
akamatwe, alitaka Aniva ashtakiwe kwa kuwabaka wasichana wadogo, lakini
hata hivyo hakuna msichana aliyejitokeza kutoa ushahidi dhidi yake.
Kwa
hivyo sasa Aniva ameshtakiwa kwa kushiriki utamaduni wenye kuumiza,
chini ya kipengee cha tano cha sheria ya usawa wa kijinsia nchini
Malawi ambapo alifanya mapenzi na wajane.
Katika kesi hii wanawake
wawili wamejitokeza ili kutoa ushahidi dhdi ya Aniva, licha ya mmoja
kusema kuwa alifanya mapenzi naye kabla ya mila hiyo kupigwa marufuku
huku mwingine naye akisema kuwa alifanikiwa kukimbia kabla ya kitendo
cha ngono kufanyika.
Hadi miaka michache iliyopita, mila hii
ilikuwa maarufu katika wilaya yote kwa mjane kufanya mapenzi na mwanamme
mara tatu kwa siku kwa usiku tatu au nne.
Eric Aniva akiwa nje ya mahakama ya Nsanje mwezi Agosti
Mwanamme huyo anaweza kuwa ndugu wa mumewe, lakini wakati mwingine mtu
kutoka nje hutafutwa kama Aniva kuweza kushiriki kitendo hicho.
Ikiwa aliyefiwa ni mwanamme, mwanamke hutafutwa kuweza kufanya mapenzi naye.
Kinachowatisha
watu nchini Malawi kuhusu Aniva, ambaye alidai kufanya mapenzi na
wanawake 104 pamoja na wasichana, wakati wa mahojiano na BBC ni kuwa
hukuachana na tabia hiyo licha ya kugundua kuwa alikuwa na virusi vya
HIV.
"HIV inaua. Itakuwaje mtu mwenye virusi kufanya kile
alichokifanya? Nafikiri yeye ni shetani. Ningekuwa hakimu ningempa
hukumu ya kifo na kifungo cha maisha," alisema mhubiri Paul Mzimu



Leave a Comment