TB JOSHUA: BI CLINTON ATASHINDA URAIS MAREKANI
Muhubiri maarufu wa vipindi vya
Televisheni nchini Nigeria TB Joshua amesema kwamba "Hillary
Clinton atamshinda Donald Trump" katika uchaguzi wa urais wenye
ushindani mkali tarehe 8 Novemba mwaka huu.
Katika ujumbe
alioutuma kwenye ukurasa wake wa Facebook TB Joshua amesema kuwa Bi
Clinton atashinda kwa ushindi mdogo, lakini atakabiliwa na changamoto
nyingini - likiwemo jaribio la kupiga kwa kura ya kutokuwa na imani
dhidi yake.
"boti ya rais mpya itakuwa imefungwa," aliongeza.
TB
Joshua ni mmoja wa viongozi wa kidini wenye ushawishi na utata barani
Afrika, huku wengi wa wafuasi wake wakiamini kuwa "utabiri " wake ni wa
uhakika.
CHANZO: BBC Swahili
Leave a Comment