MR BLUE NI SHABIKI WA DAMU WA YANGA


Imekua kitu cha kawaida sana watu mbalimbali mashuhuri kwenye sekta mbalimbali kuonesha mapenzi yao kwenye michezo. Kuanzia wanasiasa, waigizaji hadi wanamuziki.
Msanii ambaye alifanya vizuri kwenye tour ya Fiesta Mr Blue ameonekana kuwa karibu sana na club ya Yanga kwenye matukio mbalimbali ambapo inawezekana kuwepo na mapenzi makubwa na club hiyo.
Mr Blue aliwahi ku-post picha akiwa na wachezaji mashuhuri wa Yanga ambao ni Haruna Niyonzima na Simon Msuva wakiwa kwenye tukio moja usiku. Niyonzima ni mpenzi mkubwa wa bongoflava na aliwai kukiri kufatilia muziki wa Mr Blue kwa muda mrefu.
 Mr Blue ameendelea kuonyesha chembe chembe za kuwa shabiki Yanga alipo post picha akiwa ndani ya ndege amevaa T-shirt ya Yanga. Kwenye post hiyo mashabiki wake wengi kwenye comments walishikwa na hamu ya kutaka kujua uhusiano wake na club hiyo.

Inawezekana kuwa ana ushabiki wa Yanga kwasababu Mr Blue ana asili ya kuishi Kariakoo kwenye ukuaji wake ambapo sio mbali na makao makuu ya club hiyo. Watu wengine maarufu wanaoshabiki club za soka ni kama Rambo (Bolton), Katty Perry (West Ham), Jay Z (Arsenal) na wengineo.

No comments

SIRI ZA JAMII. Powered by Blogger.