MPINZANI WA MUSEVENI NCHINI UGANDA KIZZA BESIGYE, AFANIKIWA KUONDOKA UGANDA
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye ameandika kwenye
mtandao wa twitter kuwa ameondoka nchini humo licha jitihada za serikali
kumzuia.
Bwana Besigye aliliambia gazeti la Daily Monitor jana
kuwa, alilazimika kufuta safari yake kwenda nchini Afrika Kusini siku ya
Jumanne kufuatia hatua ya polisi ya kuweka kizuizi nje ya nyumba yake.
Hata hivyo msemaji wa polisi alikanusha madai hayo.
Bwana Besigye anatarajiwa kuhutubia mkutano wa tume ya kimataifa ya mawakili mjini Johannesburg siku ya Alhamis.
PATA TAARIFA KWA WAKATI:
TEMBELEA PAGE ZETU ZA FACEBOOK, TWITTER NA INSTAGRAM ZINAZOPATIKANA KWA JINA LA "SIRI ZA JAMII" NA SUBSCRIBE KATIKA BLOG YETU KUPATA TAARIFA KWA WAKATI.


Leave a Comment