MKIMBIZI KUTOKA MYANMAR AMEJIWASHA MOTO NDANI YA BANK AUSTRALIA
Mwanamume aliyejiwasha moto ndani ya Benki moja mjini Melbourne, Australia hapo jana ametambuliwa.
Yasemekana
mtu huyo anatokea Myanmar na amekuwa akitafuta hifadhi nchini
Australia. Habari zaidi zinasema aliwasili nchini humo miaka mitatu
iliyopita.
Mtu huyo mwenye umri wa miaka 21 alipelekwa hospitali kupata matibabu chini ya ulinzi wa maafisa wa usalama baada ya tukio hilo.
Wanachama wa jamii ya waislamu wa Rohingya mjini Melbourne wamesema mtu
huyo aliogopa kurudi Myanmar na kwamba alikuwa anakabiliwa na changamoto
za kimaisha.


Leave a Comment