MKE WA OBAMA AFANANISHWA NA SOKWE KATIKA CHAPISHO LA FACEBOOK HUKO WEST VIRGINIA MAREKANI
Chapisho la kibaguzi kuhusu mke wa rais wa Marekani Michelle Obama limezua utata unaomuhusu meya wa jimbo la Virginia.
Pamela
Ramsey Taylor ,ambaye anaendesha shirika moja la kihisani katika kaunti
ya Clay, alimfananisha Michelle Obama na 'sokwe' .
''Itakuwa
vyema kuwa na mtu anayefuata mitindo,mrembo na mke wa kwanza mwenye
heshima.Nimechoka kuona sokwe lililovaa viatu'',alisema.
Meya mwengine kutoka eneo hilo Beverly Whaling alijibu kwa kusema ''umeifanya siku yangu nzuri''.
Bi Beverly Whaling ni meya wa mji wa Clay ambao una idadi ya takriban watu 491.
Mji huo hauna wakaazi wa Marekani wenye asili ya Kiafrika,kulingana na idadi ya watu iliotolewa 2010.
Katika kaunti ya Clay zaidi ya asilimia 98 ya wakaazi 9,000 ni watu weupe.
Licha
ya idadi hiyo ndogo katika jimbo hilo ,chapisho hilo la facebook
lilisambaa nchini Marekani na katika vyombo vya habari vya kimataifa
huku ombi la kuwataka wanawake wote wawili kufutwa kazi likikusanya
saini 85,000.
Gazeti la The Washington post na lile la New York Daily yaliripoti
kwamba bi Taylor aliondolewa katika wadhfa wake siku ya Jumatatu.


Leave a Comment